Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mkutano wa kujadili usalama wa chakula waandaliwa Nairobi

Mkutano wa kujadili usalama wa chakula waandaliwa Nairobi

Mkutano wa wataalamu wa kujadili usalama wa chakula kwenye nchi  za mashariki na kusini mwa bara la Afrika umendaliwa hii leo mjini Nairobi nchini Kenya ambapo masuala kadha yanayohusu usalama wa chakula na sera zinazostahili kuwekwa ili kuhakikisha kuwepo upatikanaji wa chakula  yamejadiliwa.

Mkutano huo wa siku mbili unawaleta pamoja zaidi ya wataalamu 45.

Mkutano huu umendaliwa na mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa kuhusu haki ya kuwa na  chakula Olivier De Schutter ambaye anasema kuwa kujumuishwa kwa suala la haki ya kuwa na chukula kwenye katiba ni hatua kubwa ya kuhakikisha kuwepo usalama wa chakula.

(SAUTI YA OLIVIER DE SCHUTTER)