Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM walaani mauaji ya waandishi watatu nchini Syria

UM walaani mauaji ya waandishi watatu nchini Syria

Umoja wa Mataifa umetoa taarifa ya kulaani vikali mauwaji ya waandishi watatu nchini Syria na imesisitiza mamlaka za dola kuchukua hatua za haraka kuwalinda waandishi wa habari wanaripoti kwenye maeneo yenye mizozo.

Waandishi habari wawili raia wa Wingereza waliuawa Marchi 26 wakati kulipofanyika shambulizi katika mji wa Darkoush ulioko karibu na mpaka wa Uturuki. Katika siku hiyo hiyo mwandishi mwingine wa habari mpiga picha kutoka Syria aliuawa katika shambulizi nyingine uliofanyika huko upande wa mashariki.

Akielezea mauaji haya mkuu wa shirika la UNESCO Bi Irina Bokova amelaani mwendendo huyo ambao ameuita wenye kusikitisha na kukatisha tamaa kwa waandishi wa habari.