Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

IOM yawafunza maafisa wa Papua New Guinea

IOM yawafunza maafisa wa Papua New Guinea

Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na uhamiaji IOM limekamilisha mafunzo ya wiki mbili yaliyofanyika huko Papua New Guinea kwa ajili ya kukabiliana na tatizo la usafirishaji haramu.

Mafunzo hayo ambayo yamefanyika kwa ushirikiano baina ya IOM na serikali ya Papua yamewaleta pamoja jumla ya washiriki 200 ambao wanawajibika katika maeneo ya utekelezaji wa sheria na haki.

Mafunzo hayo yameendeshwa katika maeneo ya mipakani ikiwemo pia jimbo la magharibi la Sepik.

Pia yamefanyika kwenye eneo la miji mikubwa.

Yameendeshwa kuanzia mwezi February hadi March mwaka huu na kugusia maeneo muhimu ikiwemo sheria mpya iliyoasisiwa hivi karibuni inayohusiana na kukabiliana na vitendo vya usafirishaji haramu.