Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Uchaguzi utakaoandaliwa nchini Myanmar utakuwa mtihani kwa taifa hilo:Quintana

Uchaguzi utakaoandaliwa nchini Myanmar utakuwa mtihani kwa taifa hilo:Quintana

Mjumbe maalum  wa Umoja wa Mataifa kuhusu hali ya haki za binadamu nchini Myanmar Tomas Ojea Quintana amesema kuwa uchaguzi mdogo unaotarajiwa kundaliwa tarehe moja mwezi ujao nchini Myanmar utakuwa jaribio kwa hatua zilizopigwa na serikali  katika masuala ya mabadiliko ambapo viti 48 vya bunge vitawaniwa.

Bwana Ojea Quintana anasema kuwa itakuwa ni fursa muhimu kwa historia ya Myanmar akikisistiza kuwa uchaguzi huo utakuwa huru, wazi na wenye usawa.

Mjumbe huyo ameutaka utawala wa nchi hiyo kuonyesha kujitolea kwao na kuhakikisha kuwepo kwa uchaguzi wenye amani  ambao utawapa watu matumani ya kufanyaka kwa mabadiliko.

Pia ameitaka serikali  kuheshimu haki ya kujieleza na kukusanyika.