Serikali ya Syria yatakiwa kusitisha ghasia mara moja

30 Machi 2012

Mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa na muungano wa nchi za kirabu  nchini Syria Kofi Annan amesema kuwa serikali ya Syria ni lazima iwe ya kwanza kutangaza usitishaji wa ghasia na iondoe wanajeshi wake kutoka sehemu waliko raia.

Annan anasema kuwa anataraji  nao upinzani kuchukua mkondo huu mara moja ikiwa ni moja ya yale yaliyopendekezwa na mjumbe huyo kwa lengo la kumaliza mzozo wa kisiasa ulio nchini Syria.

Annan amesema kuwa hata kama serikali ya Syria imeitikia mpango huo sasa ni lazima iutekeleze .

Hata hivyo ameongeza kuwa hakuna dalili za kuonyesha kuwa pande husika zina mipango ya kumaliza ghasia zilizo nchini humo. Ahmed Fawzi ni msemaji wa Annan.

(SAUTI YA AHMED FAWZI)

 

♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter