New York yatunukiwa tuzo ya Miji ya Lee Kuan mwaka 2012

29 Machi 2012
Tuzo ya kimataifa ya Lee Kuan Yew ya miji kwa mwaka 2012 ametunukiwa meya wa jiji la New York Michael Bloomberg na idara ya usafiri, mipango miji, hifadhi na burudani limesema shirika la Umoja wa mataifa la makazi UN-HABITAT.

Waandaaji wa tuzo hiyo wamesema mji wa New York umefanya mabadiliko makubwa baada ya mashambulizi ya Septemba 11 na kuleta matumaini mapya ya mji huo.

UN-HABITAT imesema kwa kipindi kifupi mji umejengeka upya na kuongeza nakshi zinazowapa ujasiri wakaazi na watalii wanaotembelea jiji hilo.

(RIPOTI YA JASON NYAKUNDI)

 

♦ Kutembelea ukurasa maalum wa COP26 bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter