Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM watoa wito wa dola milioni 84 za kusaidia wakimbizi wa Syria

UM watoa wito wa dola milioni 84 za kusaidia wakimbizi wa Syria

Umoja wa Mataifa pamoja na washirika wake wa kutoa huduma za binadamu hii leo wametoa ombi la dola milioni 84 zitakazotumika kuwasiadia wakimbizi wa Syria walio nchini Jordan, Lebanon Uturuki na Iraq.

Mpango huo unakadiria kuwa kwa muda wa miezi sita inayokuja utahitaji kuwashughulikia wakimbizi 100,000 raia wa Syria.

Hata hivyo mpango huo hautoi shughuli zozote nchini Syria kwenyewe.

Ombi lingine kutoka kwa shirika la kuratibu masuala ya kibinadamu la Umoja wa Mataifa OCHA unatarajiwa kutolewa hivi karibuni.

Adrian Edward ni msemaji wa UNHCR.

(SAUTI YA ADRIAN EDWARD)