Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Baraza la Usalama launga mkono mageuzi ya kisiasa yatakayoongozwa na Syria

Baraza la Usalama launga mkono mageuzi ya kisiasa yatakayoongozwa na Syria

Baraza la usalama limetoa ujumbe ambao unaweza kutafsiriwa kama imara na wa pamoja kwa serikali ya Syria kuwezesha kukabiliana kwa haraka na mzozo unaoikumba nchi hiyo.

Baraza hilo jumanne lilikumbatia taarifa kwa pamoja inayounga mkono pointi 6 za mwongozo uliotolewa na Kofi Annan na tume maalum ya Umoja wa Mataifa na kamati maalum ya kiaarabu juu ya Syria.

Baraza hilo limesema kuwa mpango huo unanuia kuwezesha mageuzi ya kisiasa yalioongozwa na Syria wezesha huduma salama za kibinadamu na UM kuhakikisha kukomeshwa kwa ghasia za vikosi vilivyo jihami kwa njia zote na vikundi vyote.

Taarifa hiyo ya baraza la Usalama pia ilihimiza ushirikiano na Bw. Annan na tume yake na kusema kwamba, hatua zaidi zitachukuliwa endapo mapendekezo hayatavuna matunda.

Balozi wa Uingereza UM Mark Lyall Grant ndiye rais wa baraza la Usalama mwezi March.

Grant amesema, hii inatoa ujumbe wa kina na wa pamoja kwamba serikali ya Syria na wadau wote Syria wanapaswa kutekeleza na kutekeleza kwa haraka mpango wa pointi 6 uliowasilishwa na Kofi Annan.

Hii imekuja baada ya Urusi na China kupiga marufuku mara mbili azimio la kuishtumu Syria.