Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM walaani mauaji ya raia Afghanistan

UM walaani mauaji ya raia Afghanistan

Umoja wa Mataifa umelaani vikali tukio la mauaji ya raia huko Kusini mwa Afghanistan na kutaka malaka husika kuchunguza mwenendo wa mauaji hayo.

Duru za vyombo vya habari zimepasha kuwa, askari wa Kimarekani walioweka kambi katika jimbo la Kandahar ndiyo waliohusika na mauwaji hayo.

 Askari hao wanadaiwa kuzishambulia nyumba kadhaa na kusababisha vifo vya watu 16 wengi wao wakiwa watoto na wanawake.

Katika taarifa yake juu ya tukio hilo, Umoja wa Mataifa umesema kuwa umesononeshwa na kusikitishwa kutokana na mauaji hayo na kuitaka dola ya Afghanistan kuendesha uchunguzi dhidi ya tukio hilo.