Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mtaalamu wa UM ataka kuendeshwa uchuguzi dhidi ya Serikali ya Malaysia inayodaiwa kuwabana waandamanaji

Mtaalamu wa UM ataka kuendeshwa uchuguzi dhidi ya Serikali ya Malaysia inayodaiwa kuwabana waandamanaji

Mjumbe maalumu wa Umoja wa Mataifa anayehusika na masuala ya uhuru wa maoni ya kujieleza ametoa wito akitaka kuendeshwa kwa uchunguzi kwa serikali ya Malaysia ambayo inashutumiwa kuendesha vitendo vya kukandamiza waandamanaji wanaopigania haki ya kuwepo kwa uchaguzi huru na haki.

Kumekuwa na ripoti kwamba mwishoni mwa juma maafisa wa serikali walitumia mabomu ya kutoa machozi na maji ya kuwasha washa ili kuwatawanya waandamanaji waliokusanyika kwa amani na kusababisha kifo cha mtu mmoja.Hata hivyo mamlaka hiyo iliwatia nguvuni watu wengine 1,600 waliokuwepo kwe nye maandamano hayo ya amani .Mjumbe huyo wa Umoja wa Mataifa Frank La amesema kuwa kitendo kilichofanywa na serikali ya Malaysia kinabinya mchakato wa kukuza demokrasia na kutaka kuwepo kwa uchunguzi juu ya hali hiyo.