Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kitendo cha kuwarejesha kwa nguvu waomba hifadhi kutoka DPRK kikome:UM

Kitendo cha kuwarejesha kwa nguvu waomba hifadhi kutoka DPRK kikome:UM

Mtaalamu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa ametoa wito wa kukomesha kitendo cha kuwarejesha kwa ngvu waomba hifadhi wanaoikimbia ukiukaji wa haki za binadamu kwenye Jamhuri ya Kidemokrasia ya watu wa Korea au DPRK.

Marzuki Darusman ambaye ni mtaalamu wa haki za binadamu DPRK amezitaka nchi majirani wa DPRK kuzingatia misingi ya kutoa ulinzi wa kimataifa na kuepuka kuwarejesha kwa nguvu watu wanaoomba hifadhi. Katika ripoti yake kwenye baraza la haki za binadamu bwana Darsman amesema idadi ya watu wa Korea Kaskazini wanaoomba ukimbizi Korea ya Kusini inaongezeka na imefikia 23,700 mwishoni mwa mwaka 2011. Ameongeza kuwa wengi wa waomba hifadhi hao wamepitia adhabu kali katika makambi ya kushinikizwa kufanya kazi au wamekuwa wahanga wa vitendo vya utesaji na mifumo mingine ya unyanyasaji.

(SAUTI YA MARZUKI DARUSMAN)

Akijibu kuhusu taarifa hiyo mkuu wa ujumbe wa DPRK balozi So Se Pyong amerejea kusisitiza msimamo wa nchi yake kutotoa ushirikiano kwa mtaalamu huyo wa haki za binadamu akisema ripoti yake ni ya kisiasa na ina madai mengi yasiyo na msingi na ya uongo.