Mwakilishi wa Katibu Mkuu kuzuru Sudan Kusini

9 Machi 2012

Mwakilishi maalumu wa Katibu Mkuu juu ya masuala ya watoto na maeneo yaliyokumbwa na mizozo anatazamiwa kuzuru Sudan Kusini.

Radhika Coomaraswamy anatazamiwa kuwasili nchini humo March 11, na ataaendelea kusalia huko hadi March 17. Katika ziara yake hiyo pia atatembelea jimbo la Jonglei ambalo linaandamwa na machafuko ya kikabila mara kwa mara.

Anatazamia kutupia macho maeneo mbalimbali pamoja na kujionea namna mipango mbalimbali iliyowekwa na serikali yenye shabaha ya kuhakikisha kwamba hakuna mtoto yoyote anayetumikishwa kwenye vikosi SPLM.

Atatathmini athari zilizosababishwa na mapigano ya mipakani baina ya Sudan Kusin na Sudan Khartoum.

Atakuwa na majadiliano na wataalamu mbalimbali watakaoangazia athari zilizosababishwa na vikosi vya waasi wa LRA.

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud