Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ripoti yafichua kuwepo kwa ongezeko la watoto wanaotumbukia kwenye mazingira hatarishi

Ripoti yafichua kuwepo kwa ongezeko la watoto wanaotumbukia kwenye mazingira hatarishi

Ripoti moja inasema kiwango cha watoto watumbukiao kwenye mazingira hatarishi kinazidi kuongezeka na hivyo kuendelea kuzusha kwa hali ya sintofahamu juu ya mustakabala wao.

Ripoti hiyo inasema kuwa watoto wanaotengana na familia zao  ama kukosa mahusiano ya karibu, ndiyo wako hatarini zaidi kiasi cha kwamba kuleta wasiwasi wa kuongezeka kwa biashara ya uuzaji watoto na kutumbikia kwenye biashara ya ngono.

Mwandishi wa ripoti hiyo Najat Maalla M’jid amesema kuwa pamoja na kuwepo kwa jitihada mbalimbali za kuwakwamua watoto hao, lakini ukweli wa mambo ni kwamba kundi kubwa la watoto linaendelea kuangukia kwenye mazingira magumu.

Wengi wao wanalazimika kujiingiza kwenye kazi ngumu na hata kutumbukia kwenye mikono ya watu waendeshao biashara haramau ya uuzaji watoto ambao baadaye hugeuzwa kama sehemu ya kujiingiza fedha kutokana na kuwatumikisha kwenye kazi mbalimbali.