Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Serikali ya Pakistan yatakiwa kukomesha ghasia

Serikali ya Pakistan yatakiwa kukomesha ghasia

Wataalamu watatu wa Umoja wa Mataifa wanaohusika na haki za dini na mauaji ya kinyume na sheria hii leo wameitaka serikali ya Pakistan kuchukua hatua ili kumaliza ghasia na kuboresha usalama kwa dini ndogo kufuatia kutokea mauaji ya waumini wa dini moja mara mbili kwa muda wa majuma mawili.

Mnamo Februari 28 basi moja lilishambuliwa kwenye eneo la Kohistan kaskazini mwa Pakistan mashambulizi yanayokisiwa kutekelezwa kutoka jeshini ambapo waumiini 18 wa dhehebu la Shia waliuawa .

(Ripoti ya George Njogopa)