ICRC yatoa ombi la Euro milioni 10 kuwasaidia watu 700,000 Mali na Niger

28 Februari 2012
Chama cha kimataifa cha msalaba mwekundu na cha mwezi mwekundu ICRC kinatoa wito wa mchango wa Euro milioni 10 zitakazotumika kuwapelekea misaada watu 700,000 nchini Mali na Niger na kugharamia huduma zingine za kibinadamu kwenye mataifa hayo mawili.

ICRC inasema kuwa watu nchini Mali kwa sasa wanakabiliwa na matatizo aina mbili ikiwemo ukosefu wa chakula na mapigano ambayo yanaendelea kaskazini mwa Mali na ambayo yamesababisha kuhama kwa idadi kubwa ya watu. Steven Anderson kutoka ICRC.

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter