Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Idadi kubwa ya ndovu wauawa nchini Cameroon

Idadi kubwa ya ndovu wauawa nchini Cameroon

Katibu anayehusika na biashara ya kimataifa kuhusu sehemu na wanyama walio kwenye hatari ya kuangamia John Scanlon ameelezea hofu iliyopo kutokana na ripoti ya kuuawa kwa karibu ndovu 450 kwenye mbuga ya kitaifa ya Bouba Ndjida iliyo Kaskazini mwa Cameroon.

Serikali katika eneo hilo zimepewa usaidizi wa kuwatafuta na kuwafikisha mbele ya sheria wahusika na pia kukamata pembe za ndovu hao. Nchi zinakopelekwa pembe pia zimetakiwa kuwa macho na kutoa ushirikiano.

(RIPOTI YA GEORGE NJOGOPA)