Brazil kufadhili ununuzi wa chakula kwenye nchi tano barani Afrika

Brazil kufadhili ununuzi wa chakula kwenye nchi tano barani Afrika

Serikali ya Brazil, inatoa dola milioni 2.3 zitakazotumika kufadhili mpango wa kununua chakula uliobuniwa na shirika la kilimo na mazao la Umoja wa Mataifa FAO na lile la mpango wa chakula duniani WFP ili kuwanufaisha wakulima na watu wanaohitaji chakula kwenye nchi tano barani Afrika zikiwemo Ethiopia, Musumbiji, Niger na Senegal.

Mpango huo utanunua chakula kutoka kwa wakulima wadogo na kisha chakula hicho kitatumika kwenye programu za kulisha watoto shuleni. Kwenye makubaliano ya leo, FAO ambayo itapokea dola milioni 1.55 itawapa wakulima mbegu na mbolea na kuwasaidia wakulima hao kwa kununua na kuuza mazao yao.