Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Walioathiriwa na mvua wanahitaji msaada nchini Burundi

Walioathiriwa na mvua wanahitaji msaada nchini Burundi

Takriban watu 2000 waliolazimika kuhama makwao kufuatia mvua kubwa kwenye eneo la Gatumba lililo nje ya mji mkuu wa Burundi Bujumbura kwa sasa wanahitaji chakula na makao. Mvua hiyo iliharibu karibu nyumba 400 na kuna hofu ya kutokea kwa uharibifu zaidi kwenye maeneo yaliyoathirika yakiwemo Kinyinya , Mushasha na Muyange.

Nyumba hizo zinazungukwa na maji huku zingine zikizidi kuporomoka. Maafisa katika eneo la Gatumba wametoa wito kwa serikali na mashirika ya kutoa misaada kuzisaidia familia zilizoathirika. Walioathiriwa kwa sasa wamechukua hifadhi kwa majirani ambao nyumba zao hazikuporomoka.