Uhalifu dhidi ya ubinadamu umetendwa Syria

13 Februari 2012

Mkuu wa haki za binadamu kwenye Umoja wa Mataifa Navi Pillay amesema kuwa huenda uhalifu dhidi ya ubinadamu umetendwa nchini Syria. Akilihutubia Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa Pillay amesema kwamba zaidi ya watu 5,400 wameuawa nchini Syria tangu mikakati ya serikali ya kupambana na waandamanaji kuanza mwezi machi mwaka uliopita huku watu wengine 18,000 wakiwa kizuizini.

Pillay aliwaelezea mabalozi kuhusu hali ya haki za binadamu nchini Syria ukiwemo mji wa Homs ambao kwa sasa unazingirwa na jeshi.

(SAUTI YA NAVI PILLAY)

Ujumbe wa kutafuta ukweli, tume ya uchunguzi kuhusu Syria, na mimi mwenyewe tumeamua kuwa uhalifu dhidi ya ubinadamu huenda umetendwa nchini Syria. Nimelipa ushauri baraza la usalama kuiripoti hali nchini Syria kwenye mahakama ya kimataifa ya uhalifu wa kivita. Nchi wanachama ni lazima zihakikishe kuwa uhalifu ni lazima uadhibiwe. Uhalifu unazindi kutendwa vile ninapoendelea kuzungumza

 

♦ Kutembelea ukurasa maalum wa COP26 bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter