Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM wakaribisha hatua ya kufunguliwa mashtaka kwa afisa wa jeshi Guinea anayetuhumiwa kuhusika na ubakaji wa halaiki

UM wakaribisha hatua ya kufunguliwa mashtaka kwa afisa wa jeshi Guinea anayetuhumiwa kuhusika na ubakaji wa halaiki

Umoja wa Mataifa umepongeza na kukaribisha kwa furaha hatua ya mahakama moja nchini Guinea ambayo imemfungulia mashtaka afisa moja wa ngazi ya juu wa jeshi anayedaiwa kuhusika na vitendo vya ubakaji wakati wa maandamano makubwa ya amani yaliyofanyika katika mji mkuu wa nchi hiyo mwaka 2009.

Akiielezea hatua ya mahakama kumfungulia mashtaka afisa huyo wa jeshi, Mkuu wa Umoja wa Mataifa anayehusika na matukio ya ubakaji kwenye maeneo yaliyokumbwa na mizozo, Bi Margot Wallstrom amesema kuwa haki sasa iananza kufuata mkondo wake.

Ameeleza kuwa haki iliyocheleweshwa kwa muda mrefu, lakini kwa nukta hii iliyofikiwa sasa hakuna anayeweza kusema kuwa haki hiyo sasa imetupwa kapuni.

Maamia ya watu walipoteza maisha na wengine kujeruhiwa vibaya pale vikosi vya serikali viliposhambulia kundi la waandamanaji waliokusanyika kwenye uwanja wa mpira Mjini Conakry kupaza sauti zao dhidi ya mwendendo wa serikali

Luteni Kanali Moussa Tiegboro Camara amefunguliwa mashtaka ya mahakama ya taifa juu ya kuhusika kwake na vitendo vya kinyama ikiwemo kuendesha vitendo vya ubakaji kwa makundi ya watu.