Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

IOM yapata msaada wa kusadia waathiriwa wa tufani nchini Ufilipino

IOM yapata msaada wa kusadia waathiriwa wa tufani nchini Ufilipino

Shirika la kimataifa la uhamiaji IOM limepokea dola 202,000 zaidi kutoka kwa shirika la kimataifa la maendeleo la Canada ili kuweza kusaidia familia zilizoathiriwa na tufani kwa jina Washi nchini Ufilipino. Fedha hizo zitalisaidia shirika la IOM kutoa makao, fedha na misaada mingine kwenye miji ya Cagayan de Oro na Iligan.

Kati ya mashirika yanayochangia kwenye shughuli hiyo ni pamoja na CERF na USAID. Kwa sasa IOM imetoa makao kwa familia 1800 kwenye sehemu za Lumbia na Cagayan de Oro. Jumbe Omar Jumbe ni msemaji wa IOM.

(SAUTI YA JUMBE OMAR JUME)