Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNHCR katika jitihada za kutafuta suluhu kwa wakimbizi kwenye mataifa matatu

UNHCR katika jitihada za kutafuta suluhu kwa wakimbizi kwenye mataifa matatu

Shirika la kuhudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa UNHCR linaweka mikakati ya kumaliza tatizo la wakimbizi barani Afrika hasa tatizo la wakimbizi nchini Angola, Liberia na Rwanda. Mikakati hiyo ambayo kwanza ilitangazwa mwaka 2009 inalenga kutafuta suluhu la wakimbiz kwenye mataifa hayo matatu inayowalenga pia wakimbizi walio nchini mwao, au nchi za kigeni.

Kati ya suluhu zinatakazotolewa ni kusaidia kurejea nyumbani kwa hiari au kuwasiadiaa kuwa na vibali vya kuendelea kuishi kwenye mataifa wanayoishi sasa.