Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kaing Guek Eav ahukumiwa kifungo cha maisha gerezani

Kaing Guek Eav ahukumiwa kifungo cha maisha gerezani

Mahakama ya juu nchini Cambodia hii leo imempa Kaing Guek Eav ambaye pia anajulikana kama Duch kifungo cha Maisha gerezani ambayo ndiyo hukumu ya juu zaidi iliyo kwenye sheria kuhusu kesi za uhalifu wa kibinadamu. Mahakama hiyo ilitupilia mbali kifungo cha miaka 35 kilichotolewa na mahakama nyingine tarehe 26 mwezi Julai mwaka 2010.

Mahakama hiyo pia ilitupilia mbali rufaa iliyowasilishwa mahakamani na Kaing Guek Eav yenye madai kuwa kesi yake haikustahili kusikilizwa kwenye mahakama hiyo.