Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Makazi ya walowezi wa kiyahudi sio kitovu cha mgogoro:Netanyahu

Makazi ya walowezi wa kiyahudi sio kitovu cha mgogoro:Netanyahu

Ujenzi wa makaazi ya walowezi unaofanywa na Israel katika eneo la Wapalestina linalokaliwa sio kitovu cha machafuko Mashariki ya Kati amesema waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu.

Netanyahu ameyasema hayo kwenye mkutano na waandishi wa habari akiwa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon mjini Jerusalem kabla Ban hajaenda Gaza.

Ban amesema amemweleza waziri mkuu kwamba ujenzi wa makazi ya Walowezi hausaidii lolote kwenye mchakato wa amani na kupata suluhu ya mgogoro baina ya Israel na Palestina.

Lakini waziri mkuu Netanyahu amesisitiza kwamba suala la makazi ya Walowezi lisiwe sharti katika mazungmzo ya amani, bali liwe kama sehemu ya maafikiano ya mwisho ya amani.