Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban alaani mauwaji ya afisa wa msalaba mwekundi Syria

Ban alaani mauwaji ya afisa wa msalaba mwekundi Syria

 

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amelaani vikali mauwaji ya kiongozi wa chama cha msalaba mwenkundi nchini Syria Abd-al-Razzaq Jbeiro na ametaka wahusika wake kuchukuliwa hatua.

 Kulingana na duru za vyombo vya habari, kiongozi huyo aliuwawa kwa kupiga risasi wakati watu wasiojulikana walipolilenga gari ambalo hata hivyo lilikuwa na nembo zote za chama hicho.

Ban ameelezea masikitiko yake na ameitaka serikali ya Syria kuanzisha uchunguzi juu ya mtekelezaji wa shambulio hilo na hatimaye kufikishwa kwenye mkono wa sheria.

Katika ujumbe wake kufuatia mauwaji hayo, Ban aliikumbusha jamii namna inavyopaswa kuheshimu na kuwalinda watu ambao wamejitolea kutekeleza majukumu ya usamaria mwema.