Balozi Mulamula aliaga kongamano la maziwa makuu

27 Januari 2012

Balozi Liberata Mulamula aliyekuwa katibu mkuu wa Kongamano la kimataifa la maziwa makuu amekamilisha muhula wake wa miaka mitano kwenye uongozi wa shirika hilo linalojumuisha nchi 11 za ukanda wa maziwa makuu na ambalo dhamira yake ni kuimarisha eneo hilo hasa kuhakikisha amani na utulivu baada ya kukumbwa na migogoro mikubwa na vita jambo ambalo limekuwa likipewa pia uzito mkubwa na Umoja wa Mataifa.

Bi Mulamula raia amemkabidhi kijiti cha madaraka wiki hii kwa Profesa Alphonse Luaba Ntuba kutoka Jamhuri ya kidemorasia ya Congo kwenye makao makuu ya shirika hilo mjini Bujumbura.

Umoja wa Mataifa umekuwa ukipongeza kazi na juhudi kubwa za balozi Mulamula na nchi zote za maziwa makuu kwa kuonyesha nia ya kuhakikisha amani na utulivu wa kudumu inarejea maziwa makuu.

Kwa upande wake Balozi Mulamula amesema kuna baadhi ya mafanikio yaliyopatikana ikiwepo uundwaji wa taasisi hiyo kiasi cha kukubalika kimataifa na eneo la maziwa makuu lakini pia kuanza kushuhudia utulivu ingawa ameonya kwamba bado kuna changamoto ya mabaki ya makundi ya wapiganaji na waasi.

Muandishi wetu wa maziwa Ramadhani Kibuga amezungumza na Balozi Liberata Mulamula ambaye yuko katika pilka za kufungasha mizigo yake kurejea nyumbani Tanzania, ungana nao.

(SAUTI YA RAMADHAN KIBUGA NA MULAMULA)

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter