Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Afisa wa UM ataka Israel na Palestina kutatua shida zao

Afisa wa UM ataka Israel na Palestina kutatua shida zao

 

Afisa wa masuala ya kisiasa kwenye Umoja wa Mataifa amezishauri Israel na utawala wa Palestina kuweka juhudi ili kutatua tofauti zilizo kati yao na kubuni taifa huru la kipalestina litakalokaa pamoja kwa amani na Israel.

Akilifahamisha Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuhusu hali ya mashariki ya kati naibu katibu katika masuala ya kisiasa kwenye Umoja wa Mataifa Oscar Fernandez-Taranco amesema kuwa uongozi unahitajika kuhakikisha kuwa mpango wa kutafuta amani unasonga mbele. Amesema kuwa jamii ya kimataifa itachukua hatua ili kuunga mkono jitihada za kupatikana kwa suluhu la mzozo uliopo kwa njia ya amani.