Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mlipuko wa bomu watokea katika kambi ya wakimbizi Moghadishu

Mlipuko wa bomu watokea katika kambi ya wakimbizi Moghadishu

Taarifa kutoka kambi ya wakimbizi mjini Moghadishu Somalia zinasema kumetokea mlipuko wa bomu muda mfupi baada ya kuwasili ujumbe wa waandishi wa habari wa kigeni ulioambatana na maafisa wa Umoja wa Mataifa waliokuwa wanazuru kambi hiyo.

Kwa mujibu wa Yasmin Ali afisa wa kambi hiyo watu wawili wameuawa katika mlipuko huo uliotokea Alhamisi, mmoja mkimbizi na askali wa jeshi la Somalia.

Miongoni mwa waandishi wa habari waliozru kambini hapo ni kutoka AFP, BBC na gazeti la Hispania la El Pais ambao walikuwa katika ziara ya siku moja miezi sita baada ya Umoja wa Mataifa kutangaza njaa Somalia. Ari Gaitanis mwandishi wa habari wa Umoja wa Mataifa anasema bado ni mapema mno kubaini nini hasa kilichosababisha mlipuko huo na nani aliyehusika.

(SAUTI YA ARI GAITANIS)