Umoja wa mataifa wataka kupelekwa misaada zaidi nchini Somalia

Umoja wa mataifa wataka kupelekwa misaada zaidi nchini Somalia

Umoja wa Mataifa pamoja na washirika wake wametoa wito wa kutaka kuendelea kuwepo usaidizi kwa oparesheni za kibinadamu kwenye pembe ya Afrika hata kama inakabiliwa na changamoto katika usambazaji wa misaada kwa wanayoihitaji nchini Somalia.

Akiongea mjini Geneva mratibu wa Umoja wa Mataifa nchini Somalia Mark Bowden amesema kuwa hata kama watu nusu milioni wameokolewa kutoka kwenye hatari ya kuangamia idadi ya wanaohitaji usaidizi bado inasalia ya juu hadi watu milioni nne. Bowden amesema kuwa kuna haja ya kutumia njia zingine za kuisaidia Somalia ikiwemo kuzisaidia jamii kurejea shughuli za kilimo na ufugaji.

(SAUTI YA MARK  BOWDEN)

Naye Rita Maingi Afisa wa OCHA Nairobi akizungumza na Radio ya UM anasema.

(SAUTI YA RITA MAINGI)