Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Azimio la UM la Januari 1942 lililomng'oa Hitler latimiza miaka 70

Azimio la UM la Januari 1942 lililomng'oa Hitler latimiza miaka 70

Umoja wa Mataifa unaadhimisha miaka 70 ya azimio muhimu la kidiplomasia kufuatia vita vya pili vya dunia ambalo lilichagiza kuundwa kwa Umoja wa Mataifa.

Azimio hilo lililojulikana kama “1942 UN Declaration” lilitiwa saini na mataifa 26 yakiwemo ambayo yaliyojulikana wakati huo kama washirika wakubwa wanne ambao ni Marekani, Uingereza, Muungano wa Soviet na Uchina.

Washirika hao wanne walikuja pamoja ili kumaliza vita dhidi ya tawala za kiimla na kijeshi za Ujerumani, Italia na Japan. Dan Plesch ni mkurugenzi wa kitivo cha mafunzo ya kimataifa na diplomasia kwenye shule ya mafunzo ya Mashariki na Afrika mjini London. Plesch anasema misingi hiyohiyo bado inauongoza Umoja wa Mataifa hii leo.

(SAUTI YA DAN PLESCH)