Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

IOM yawasaidia raia wa Haiti waliokimbilia Jamhuri ya Dominica kurudi nyumbani

IOM yawasaidia raia wa Haiti waliokimbilia Jamhuri ya Dominica kurudi nyumbani

Baada ya tetemeko kubwa la ardhi kuikumba Haiti Januari mwaka uliopita karibu watu 200,000 raia wa Haiti walivuka na kuingia kwenye Jamhuri ya Dominica wakitafuta matibabu na ajira huku wengine wakikimbia hali iliyofuata tetemeko hilo. Lakini hata hivyo wengi wameamua kurejea nchini Haiti.

Shirika la kimataifa la uhamiaji IOM limewasaidia wanaotaka kurejea nyumbani kwa hiari kwa ushirikiano idara ya uhamiaji nchini Dominica na polisi.