Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

FAO na EU kuchagiza kilimo kinachozingatia mabadiliko ya hali ya hewa

FAO na EU kuchagiza kilimo kinachozingatia mabadiliko ya hali ya hewa

Shirika la chakula na kilimo la Umoja wa Mataifa FAO na muungano wa Ulaya EU Jumatatu wametangaza mradi mpya utakaogharimu Euro milioni 5.3 kuzisaidia Malawi, Vietnam na Zambia katika kipindi cha mpito kuelekea mtazamo mpya wa kilimo unaozingatia hali ya hewa.

Jamii ambazo zinategemea sana kilimo kwa maisha na usalama wa chakula ziko katika hatari kutokana na mbadiliko ya hali ya hewa, na wakati huohuo kilimo ambacho ni mzalishaji mkubwa na gesi ya viwandani kinachangia katika mabadiliko ya hali ya hewa.

FAO na EU wanasema mtazamo mpya katika kilimo utasaidia kuifanya sekta hiyo kutumika kama suluhisho la changamoto kubwa, lakini pia kusaidia katika kupambana na umasikini na njaa, kupunguza gesi chafu na kukabili mabadiliko ya hali ya hewa.