Kenya yaitaka Baraza la Usalama kutoa msaada zaidi katika suala la Somalia

13 Januari 2012

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa wiki hii imepokea ombi lililowasilishwa na serikali ya Kenya na muungano wa Afrika, wa kuchukua hatua zaidi kisaidia Somalia. Serikali ya Kenya pia imesema iko tayari kupeleka vikosi vya kujiunga na vikosi bvya kulinda amani vya muungano wa Afrika AMISOM kulikomboa taifa hilo la Pembe ya Afrika lililoghubikwa na vita kwa zaidi ya miongo miwili.

Waziri wa mambo ya nje wa Kenya Moses Wetangula ambaye pia ni mwenyekiti wa baraza la amani na usalama la muungano wa Afrika amelitaka baraza hilo kuidhinisha kupanuliwa wigo wa AMISOM. Katika mjadala huo uliojumuisha wajumbe wote 15 wa Baraza la Usalama wamejadili pia suala la kumaliza kipindi cha mpito, kuunda katika mpaya na kuchagua Rais na wabunge wa serikali mpya. Flora Nducha ameketi na waziri Wetangula kufafanua ajenda walizojadili.

(MAHOJIANO NA WAZIRI WETANGULA)

Kwa upande wake Baraza la Usalama linaunga mkono jitihaza zote za khakikisha Somalia inapata amani ya kudumu ambayo pia itakwa afueni kwa jirani zake wote wa Pembe ya Afrika. Limeitaka jumuiya ya kimataifa kujitoa kimasomaso kuhakikisha nia hiyo inatimizwa, lakini imesisitiza kwa ukarimu huanzia nyumbani. Maite Nkoana Mashabane ni Waziri wa mambo ya nje wa Afrika ya Kusini ambaye pia ni Rais wa Baraza la Usalama kwa mwezi huu.

(SAUTI YA MAITE MASHABANE)

 

♦ Kupata takwimu za waathirika vitani Ukraine bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter