Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Hatma ya amani DRC, macho na masikio yaelekezwa Addis Ababa

Hatma ya amani DRC, macho na masikio yaelekezwa Addis Ababa

Hali ya usalama Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo, DRC imeendelea kuwa gumzo kila uchwao kutokana na mazingira yasiyotabirika, ambayo hufanya wakazi wake kuendelea kuwa wakimbizi ndani ya nchi yao iliyosheheni rasilimali lukuki; chini ya ardhi na juu ya ardhi. Katika eneo hilo vikundi vya waasi kikiwemo kile cha M23 kimekuwa kikisababisha hofu miongoni mwa wakazi huku jeshi la nchi hiyo likielezwa kuwa na uwezo mdogo kukabiliana nao.  Hata hivyo nuru inaonekana kuingia wakati huu ambapo Jumapili ya tarehe 24 mwezi Februari makubaliano yanatarajiwa kutiwa saini ili kupatia suluhu mzozo huo. Basi katika makala yetu wiki Assumpta Massoi anamulika safari ya kuelekea utiwaji saini kwa makubaliano hayo.