Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

India imetimiza mwaka mmoja bila kuwa na visa vya Polio

India imetimiza mwaka mmoja bila kuwa na visa vya Polio

India imetimiza mwaka mmoja bilia kuwa na visa vya polio tangu kisa cha mwisho kiliporekodiwa kwa mtoto wa miaka miwili jimbo la West Bengali Januari 13 mwaka 2011.

India kuna wakati ilitambulika kama kitovu cha ugonjwa wa polio duniani, na viongozi wa afya duniani hii leo wameipongeza serikali ya India kwa jitihada zake, uongozi wake na kutenga fedha muafaka kupambana na kutokomeza polio. Nchini humo kila mwaka watoto zaidi ya milioni 170 wa chini ya umri wa miaka mitano wanapata chanjo katika awamu mbili za kitaifa za chanjo.

Kwengineko duniani visa vya polio vinaendelea zikiwemo nchi za Afghanistan na Pakistan vimerejea, na Afrika Nigeria, Chad na Jamhri ya Kidemokrasia ya Congo huku kukiwa na mlipuko mpya Jamhuri ya Afrika ya Kati. Sona Bari ni afisa uhusiano wa mambo ya nje wa mpango wa kimataifa wa kudhibiti polio wa WHO.

(SAUTI YA SONA BARI)