Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Syria yalaumu mataifa ya nje kwa kuchochea ghasia nchini mwake

Syria yalaumu mataifa ya nje kwa kuchochea ghasia nchini mwake

Mamlaka nchini Syria imesisitiza kuwa machafuko yanayoendelea kujiri sasa nchini humo yanamkono toka mataifa ya nje. Vuguguvu la maandamano ya amani ya kupinga utawala wa rais Bashar al-Assad yamepinduka na kugeuka uwanja wa vita.

Balozi wa Syria kwenye Umoja wa Mataifa Bashar Ja’afari amesema kuwa baadhi ya maafisa kutoka mataifa ya kigeni wanapenyeza ushawishi wa chini kwa chini wakiyataka makundi ya kijeshi kutoachana na matumizi ya vita na wala kutojiingiza kwenye meza ya majadiliano.

Balozi huyo amewaambia waandishi wa habari kuwa mamlaka ya Syria inahuzunika juu ya kuendelea kuuwawa kwa mamia ya raia wakati huu.