Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Shirikisho la msalaba mwekundu duniani kuadhimisha miaka 2 ya tetemeko la Haiti

Shirikisho la msalaba mwekundu duniani kuadhimisha miaka 2 ya tetemeko la Haiti

Wakati shirikisho la msalaba mwekundu duniani likijiaandaa kuadhimisha mwaka wa pili hapo January 12 tangu kutokea kwa tetemeko kubwa la ardhi nchini Haiti, taarifa ya shirikisho hiyo imepongeza kuimarika kwa mifumo ya kijamii nchini humo na kusema kuwa watu waliokosa makazi na kulazimika kuishi kwenye mahema maalumu sasa idadi yao imepungua.

Katika taarifa yake, shirikisho hilo la msalaba mwekundu limesema kuwa idadi ya watu waliokosa makazi kutokana na nyumba zao kuharibiwa na tetemeko hilo imepungua kwa kiwango cha kuridhisha.

Imesema idadi yao imepungua kutoka watu milioni 1.5 hadi kufikia chini ya watu 550,560 . Hadi sasa eneo hilo limesalia na mahema yanayofikia 802 toka yale ya awali yaliyokuwa 1,555.

Hata hivyo shirikisho hilo limesema kuwa bado kuna hali ya mkwamo wa hapa na pale inayotatiza kwa wengi kurejea kwenye hali zao za kawaida, lakini imehaidi kuendelea kuzikabili changamoto zilizopo.