Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Yousssou N’Dour aacha kuhudumu kama balozi mwema wa UNICEF

Yousssou N’Dour aacha kuhudumu kama balozi mwema wa UNICEF

Shirika la kuhudumia watoto la Umoja wa Mataifa UNICEF limetangaza kuwa mwanamuziki maarufu duniani Youssou N’Dour ameuacha kwa muda wadhifa wake kama balozi mwema wa shirika hilo wakati anapoendelea na kampeni yake kuwania urais nchini Senegal.

Kulingana na sera za UNICEF wanasiasa au wanaowania wadhifa kwenye serikali hawawezi kuhudumu kama mabalozi wema wa shirika hilo. UNICEF imefaidika kutoka kwa huduma za bwana N’Dour hivi majuzi hasa alipotembelea watoto kwenye kambi ya Dadaab kaskazini mwa Kenya Septemba mwaka 2011.