Wanawake wapiga hatua katika upatanishi:UM

Wanawake wapiga hatua katika upatanishi:UM

Naibu katibu katika kitengo cha Umoja wa Mataifa kinachohusika na masuala ya kisiasa Lynn Pascoe amesema kuwa Umoja wa Mataifa umepiga hatua katika jitihada zake za kuwashirika wanawake kwenye masula ya kutafuta mapatano wakati wa mizozo.

Akiongea kwenye kungamano la kila mwaka la taasisi inayohusika na usalama mjini Washington DC nchini Marekani Pasceo amesema kuwa hata hivyo inahitaji wanawake zaidi kushiriki katika zeizi la upatikanaji wa amani hususan kutoka pande zote zinazozozana.

Waliohudhuria mkutano huo ni pamoja watunzaji sera kutoka mji wa Washington DC wakiwemo wanawake 20 kutoka sehemu mbali mbali za dunia walio na tajriba ya juu katika masuala ya upatanishi. Bwana Pascoe amesema kuwa Umoja wa Mataifa haswa katibu mkuu wanalipa swala la kuwashirika wanawake kwenye utatuzi wa mizozo umuhimu mkubwa.