Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mkuu wa Shirila la UNHCR kuzuru Sudan Kusini mwishoni mwa juma

Mkuu wa Shirila la UNHCR kuzuru Sudan Kusini mwishoni mwa juma

Mkuu wa shirika la kuhudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa UNHCR Antonio Guterres anatarajiwa kusafiri kwenda nchini Sudan Kusini mwishoni mwa juma hili ambapo atatembelea kituo cha wakimbizi kwenye eneo la Maaban na baadaye kusafiri kwenda Sudan ya kati tarere 10 na 13 mwezi huu.

UNHCR inasaidia serikali ya Sudan Kusini kuwachukua karibu watu 660,000 waliorejea nyumbani wakiwemo raia 360,000 wa Sudan Kusini waliotoka Sudan na wengine 300,000 waliorejea Sudan Kusini kutoka nchi zingine majirani. Mapigano ya hivi majuzi kwenye majimbo ya Blue Nile na Kordofan Kusini yamewalazimu karibu watu 75,000 kuvuka mpaka na kuingia majimbo ya Unity na Blue Nile nchini Sudan Kusini.