Afisa wa UM aridhishwa na kurejea kwa watu makwao nchini Libya

5 Januari 2012

Afisa wa ngazi ya juu kwenye Umoja wa Mataifa ambaye ametembelea miji Bani Walid, Sirte na Misrata ambayo ilishuhudia mapigano makubwa zaidi wakati wa kampeni ya kumuondoa madarakani rais Muammar Qadhafi ameelezea kuridhishwa kwake kutokana na kurejea makwao kwa watu waliokimbia mapigano hayo.

Georg Charpentier mratibu wa masuala ya kibinadamu nchini Libya ambaye alitembelea miji hiyo juma hili aligundua kuwa asilimia 60 ya watu waliohama makwao kutokana na mapigano walirejea miji ya Bani Walid na Sirte. Akiitembelea miji hiyo mratitu bwana Charpentier alikutana na wanachama wa mabaraza ya kijeshi na kutembelea maghala kwenye mji wa Bani Walid kuona usambazaji wa misaada unaofanywa na shirika la mpango wa chakula duniani WFP.

 

♦ Kutembelea ukurasa maalum wa COP26 bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter