Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban ampongeza Kiir kwa jitihada zake za kulinda raia

Ban ampongeza Kiir kwa jitihada zake za kulinda raia

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amefanya mazungumzo na rais wa Sudan Kusini Salva Kiir akimpongeza kwa kujitolea kwake katika kuwalinda raia na kwenye jitihada zake za kutafuta suluhu kwa mzozo unaondelea kati ya jamii ya Lou Nuer na Murle kwenye jimbo la Jonglei.

Kwenye taarifa iliyotolewa kupitia kwa msemaji wake baada ya mazunguzo yaliyofanywa kwa njia ya simu Ban amesema kuwa kujitolea katika kuhakikisha kuheshimiwa kwa sheria na haki za binadamu ni jambo muhimu. George Njogopa na Tarifa kamili.

(SAUTI YA GEORGE NJOGOPA)

CLIP