Serikali ya Sri Lanka yapambana na ugonjwa wa Kidingapopo

29 Disemba 2011

Maafisa wa afya nchini Sri Lanka wamesema kuwa wanafanya jitihada katika kupambana na ugonjwa unaosambazwa na mbu wa kidingapopo. Afisa katika wizara ya afya Pabha Palihawadana anasema kuwa kwa muda wa miaka miwili jitihada zimefanyika jitihada ili kuzuia kusambaa kwa ugonjwa huo na sasa matunda yameanza kuonekana.

Mwaka 2011 visa 26,722 viliripotiwa kutoka visa 34,105 vya mwaka 2010 huku idadi ya waliokufa ikipungua mkutoka watu 246 hadi watu 172. Monica Morara anaripoti.

(SAUTI YA MONICA MORARA)

 

♦ Kutembelea ukurasa maalum wa COP26 bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter