Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Brazil imeangazia wajibu wake wa kidiplomasia katika kuzuia migogoro

Brazil imeangazia wajibu wake wa kidiplomasia katika kuzuia migogoro

 

Taifa la Brazil limeangazia wajibu wake katika masuala ya dilplomasia kwa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa. Akiongea wakati wa kukamilika kwa muda wa miaka miwili kama mwanachama asiye wa kudumu wa baraza hilo balozi wa Brazil kwenye Umoja wa Mataifa Maria Luiza Ribeiro Viotti amesema kuwa Brazil imesaidia katika kuzuia mizozo kwenye sehemu nyingi za dunia ikiwemo Sudan Kunisi.