Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Haki za washitakiwa ziheshimiwe Kyrgyzstan:Pillay

Haki za washitakiwa ziheshimiwe Kyrgyzstan:Pillay

Kamishina Mkuu wa Haki za Binadamu Navi Pillay Alhamisi ameelezea masikitiko yake kuhusu mahakama kuu ya Kyrgyzstan hapo Desemba 20 kuzingatia uamuzi wa hukumu na kifungo cha maisha jela kwa mtetezi wa haki za binadamu Azimjan Askarov, licha ya ripoti kwamba aliteswa akiwa rumande na haki zake za kuwa na kesi inayofuata haki.

Askarov mkurugenzi wa shirika la kutetea haki za binadamu la Vozkukh alihukumiwa kifungo cha maisha na kupokonywa mali zake Novemba 2010 kwa makosa ya mauaji ya asifa wa polisi, kushiriki na kuandaa ghasia na kuchochea chuki za kikabila.

Kukamatwa kwa Askarov kunaaminika kuhusiana na shughuli zake za amani za kutetea haki za binadamu hususan kutanabaisha kuhusu machafuko ya kikabila katika jimbo la Jalal-Abad mwezi Juni mwaka 2010. Jason Nyakundi na ripoti kamili

(RIPOTI YA JASON NYAKUNDI)