Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

IOM yawapa makao wasomali 30,000

IOM yawapa makao wasomali 30,000

Shirika la kimatifa la uhamiaji IOM limekamilisha shughuli ya kuweka hema 8,315 ili kutoa makao kwa wasomali 30,000 waliohama makwao kutokana na ukame na ambao hawakuwa na uwezo wa kupata makao kwenye kambi ya wakimbizi ya Daadab kutokana na kuwepo msongano.

Mahema hayo yamewekwa kwenye kituo kilichobuniwa cha IFO 2 kilicho karibu na kambi Dadaab ambayo kwa sasa ni makao ya wakimbizi 383,000. Wakimbizi kutoka Somalia wamekuwa wakiwasili kwenye maeneo ya Kaskazini Mashariki mwa Kenya tangu mapema mwaka huu kufuatia kuwepo ukame na njaa sehemu kadha za nchi. Jumbe Omari Jumbe ni afisa wa IOM.

(SAUTI YA JUMBE OMAR JUMBE)