Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Nchi zilizoendelea zatakiwa kutimiza ahadi ya kimaendeleo

Nchi zilizoendelea zatakiwa kutimiza ahadi ya kimaendeleo

Maafisa wa Umoja wa Mataifa wamezitolea mwito nchi zilizoendelea kutimiza ahadi zao za misaada ya kimaendeleo kwa nchi zinazoendelea kwa kuonya kwamba kushindwa kufanya hivyo nchi hizo zinakaribisha janga jipya hasa katika kipindi hiki kinachoshuhudia mkwamo wa kiuchumi.

Maafisa hao wamesisitiza kuwa hali ya uchumi wa uchimi wa dunia unaweza kupangalanyika na tena kupoteza mwelekeo wake iwapo mataifa hayo yaliyoendelea hayataamka kutekeleza ahadi zao.

Mmoja wa maafisa hao wa Umoja wa Mataifa ambaye ni rais wa baraza kuu Bwana Nassir Abdulaziz Al-Nasser amesema kuwa hizo zipo kwenye mtego mkubwa wa kusaka majibu ya matatizo ya ndani kama vile kukabili umaskini, kufufua ajira, lakini katika upande wa pili zinapaswa kufikiria mashirikiano toka upande wa pili. Pia ametaka kuwepo kwa hali ya usawa kwenye biashara akisema kuwa kuna ulazima kufuta mfumo wa biashara unaopendelea zaidi upande mmoja.