Skip to main content

Ufadhili wa mabadiliko ya hali ya hewa usiongeze mzigo wa madeni ya nje kwa nchi maskini:UM

Ufadhili wa mabadiliko ya hali ya hewa usiongeze mzigo wa madeni ya nje kwa nchi maskini:UM

Mtaalamu huru wa Umoja wa Mataifa kuhusu madeni ya nje na haki za binadamu Sephas Lumina ameutaka mkutano wa mabadiliko ya hali ya hewa unaoendelea mjini Durban Afrika ya Kusini kuhakikisha kwamba ufadhili wa fedha uliopendekezwa hautoongeza mzigo wa madeni ya nchi kwa nchi masikini zitakazopokea ufadhili huo.

Bwana Lumina pia ametoa wito kwa kamati maalumu iliyoundwa kwa ajili ya mfuko wa ufadhili wa hali ya hewa na wawakilishi katika mkutano huo wa COP17 kuhakikisha fedha zinazotolewa kwa nchi zinakwenda sambamba na mtazamo wa nchi hizo na kuchagiza ushiriki unaohitajika wa wadau wote zikiwemo jamii, wakulima, wafanyakazi, wanawake na makundi mengine. Alice Kariuki na taarifa kamili.

(RIPOTI YA ALICE KARIUKI)