Ban akaribisha kuanza upya kwa majadiliano baina ya Serbia na Kosovo juu ya mzozo wa mpaka

7 Disemba 2011

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amekaribisha kuanza upya kwa majadiliano yanayoungwa mkono na Umoja wa Ulaya baina ya Serbia na Kosovo juu ya mzozo wao wa muda mrefu kuhusiana na mpaka. Pande hizo sasa zimekubaliana kutekeleza maazio yaliyoratibiwa na Umoja wa Ulaya maazio ambayo yanafungua njia juu ya kufikiwa kwa suluhu ya kudumu.

Akiweka zingatio lake, Ban amesema kuwa anaamini pande zote zitafikia makubaliano ambayo yataleta mwanga mpya. Mzozo wa mpaka kwa pande zote mbili umekuwa kitovu cha machafuko ya mara kwa mara na kusabisha baadhi ya watu kupoteza maisha.

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud