Ghasia za uchaguzi mkuu nchini DRC hazitavumiliwa:Ocampo

6 Disemba 2011

Wananchi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo wanaposubiri matokeo ya kura ya urais na ubunge  iliyopigwa wiki iliyopita, mwendesha mashtaka wa mahakama ya kimataifa inayohusika na uhalifu wa kivita ICC Luis Moreno-Ocampo ameonya kwamba ghasia zozote zitakazotokea zitachunguzwa na wahusika kuchukuliwa hatua.

Luis Moreno-Ocampo amesema kuwa anaendelea kupokea ripoti za mashambulizi dhidi ya raia kutoka kwa makundi yaliyojihami na jeshi. DRC ilipiga kura za urais na ubunge tarehe 28 mwezi Novemba ukiwa ndio uchaguzi wa pili kufanyika nchini humo tangu ipate uhuru.

 

♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter